Skip to main content

NI YEYE..MTUNZI ALLY KHELEF

 







       LEO,  Tutajifunza na kuburudika na utungaji wa mashairi ya kiswahili kutoka kwa mtunzi wetu Bwana ALI ABEID KHELEF......Karibu..!!

SHAIRI; NI YEYE

     Nazizima nikizani, cha kale kujitunzia, 

meingia mahabani, wavyele wanizuia, 

Nimpendae Fulani, mtima kauhamia, 

                     NI YEYE!!


Kwake yeye ni peponi, tayari nimeingia, 

Wazaziwe hawaoni, thamani kunipatia, 

Awe wangu wa ndoani, nusu dini kutimia, 

                    PINGAMIZI


Pendo langu mashakani, nahisi linapotea, 

Latanga tanga njiani, angani likielea, 

Kumkosa muhisani, moyo utanyong'onyea, 

                        MAUMIVU.!

Katika shairi hili fupi ambalo dhamira yake kuu ni tatizo kubwa ambalo watu mbali mbali huwakumba pale wanapoamua kwa moyo mkunjufu kuipalilia miti yao ya matunda lakin hukutana na vipingamizi kutoka kwa wazazi kutokana na sababu mbali mbali kama vile udini, ukabila, siasa, kipato, na mengine mengine ambayo hukata uzi wa pendo zito la wapendanao ambapo, wawili walioshibana hupelekea mifarakano ndani ya jamii.....na chuki endelevu zisizokwisha ndani yamii........TUBADILIKE...

Comments

  1. Mahaba kua makini,ndoani utajalia.
    Vishilingi mfukoni, visiwe vyakuzuzua.
    Watamani wa fulani, jipange utaumia.
    Ni maneno ya Thamani, zingatia na Tambua

    ReplyDelete
    Replies
    1. pendo kulitathmini, wengi hawajatambua,
      maneno yawe laini, laasivyo wapotea,
      kupenda si jambo geni, wa kwanza mimi sikuwa,
      sijamwona wa fulani, huru nilipo chagua,
      KAJUJU

      Delete
  2. Usiwe mtu auni, mwezako kumtishia,
    Hakuna wa fulani, ndoani hajaingia,
    Mwezako yupo tabani, kwa X ametulia,
    Kama fulani ni wko, ndoani ngeshamuweka.
    KAJUJU

    ReplyDelete
  3. Hujui ulisemalo, yafaa kulichungua,
    Nateta shika shikilo, tengua tena tengua,
    Kujua nilishikalo, yataka kufatilia,
    Pendo napima kwa kilo, wallahi nafurahia,

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

CLASSROOM ENGLISH: 300+ CLASSROOM PHRASES FOR ENGLISH TEACHERS

Pic. ( Hakielimu) Hello.! learners, Today we will look at the Important classroom phrase for English teachers, I think it will be helpful for all student/teachers, especially who take English study for teaching, Welcome here we go. Acknowledge thank yo u. GREETING / WELCOMING PHRASE Hello, everyone. Good morning, everybody. Good afternoon , class. Hello there, Tom. Good afternoon, everybody. How are you  today? How are you getting on? How’s life? How are things with you? Are you feeling better today, David? What a lovely day! What a rainy day! Today is very cold, isn’t it? ntroductions My name is Mr/Mrs/Ms Smith. I’ll be teaching you English this year. I’m your new English teacher. I’ve got five lessons with you each week  Time to begin Let’s begin today’s lesson. Let’s begin our lesson now. I hope you are all ready for your English lesson. I think we can start now. Is everybody ready to start? Now we can get down to work. It’s time to begin, please stop talking. I’m waiting ...